Tunakuletea mpango wa Google Play Pass
Pasi ya kufikia mamia ya michezo na programu bora, hamna matangazo wala ununuzi wa ndani ya programu. Watumiaji wapya wanaweza kuanza kwa jaribio lisilolipishwa, kisha watalipa bei nafuu kila mwezi. Pia upo usajili wa kila mwaka.1
Uko tayari kuanza?
Tembelea Duka la Google Play kwenye kifaa chako cha Android ujisajili1
Fungua programu ya Duka la Google Play
Gusa aikoni ya wasifu, kisha Play Pass
Maswali Yanayoulizwa Sana
Google Play Pass inagharimu pesa ngapi?
Gharama za Google Play Pass ni TSh 4,250.00 kwa mwezi na TSh 38,000.00 kwa mwaka nchini Tanzania na wasimamizi wa familia wanaweza kushiriki uwezo wa kufikia na hadi wanafamilia wengine watano.2
Ina programu na michezo gani?
Google Play Pass ina mamia ya michezo na programu, tunazidi kuweka mipya kila mwezi. Angalia Duka la Google Play kwenye kifaa chako cha Android ili upitie orodha.
Je, ninahitaji kifaa cha Android?
Ndiyo, Google Play Pass inaweza kutumiwa kwenye vifaa vya mkononi na kompyuta kibao kwa kutumia toleo la Duka la Google Play la 16.6.25 au jipya zaidi na toleo la Android la 4.4 au jipya zaidi. Pia utahitaji Akaunti ya Google inayotimiza masharti (isiwe inayosimamiwa na mzazi, shule au shirika jingine) ili ujisajili.
Ninaweza kupata maelezo zaidi wapi?
Unaweza kuangalia makala yetu ya kituo cha usaidizi ili upate maelezo zaidi kuhusu utaratibu wa Google Play Pass, jinsi ya kuanza kushiriki na familia na mengine.
Wasanidi programu wanaweza kujihusisha vipi?
Iwapo unabuni programu au mchezo ambao unafikiri kuwa utafaa kwenye Google Play Pass, unaweza kupata maelezo zaidi na kujaza fomu hii ili utume ombi la kushiriki.