Fiji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Matanitu Tu-Vaka-i-koya ko Viti
फ़िजी गणराज्य
فِجی رپبلک

Jamhuri ya Visiwa vya Fiji
Bendera ya Fiji Nembo ya Fiji
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: "Rerevaka na Kalou ka Doka na Tui"
"Umwogope Mungu na umheshimu malkia"
Wimbo wa taifa: God Bless Fiji
Lokeshen ya Fiji
Mji mkuu Suva
18°10′ S 178°27′ E
Mji mkubwa nchini Suva
Lugha rasmi Kiingereza, Kifiji na Kihindustani (Hindi/Urdu)
Serikali
Rais
Waziri Mkuu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Machifu
Jamhuri chini ya kamati ya kijeshi
Ratu Epeli Nailatikau
Frank Bainimarama
Ratu Ovini Bokini
Uhuru
Tarehe
10 Oktoba 1970
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
18,274 km² (ya 155)
--
Idadi ya watu
 - Julai 2006 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
905,949 (ya 156)
46/km² (ya 148)
Fedha Fijian dollar (FJD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+12)
(UTC)
Intaneti TLD .fj
Kodi ya simu +679

-


Shujaa wa Mlimani kutokea Fiji

Fiji (Kifiji: Matanitu ko Viti; Kihindustani: फ़िजी, فِجی) ni nchi ya visiwani ndogo ya Melanesia katika Pasifiki yenye visiwa 322 na wakazi 844,330.

Fiji iko mashariki kwa Vanuatu, magharibi kwa Tonga na kusini kwa Tuvalu.

Kati ya visiwa vingi kuna 106 vyenye wakazi. Visiwa vikuu ni Vanua Levu na Viti Levu wanapokaa asilimia 87 za wakazi wote.

Mji mkuu ni Suva.

Lugha rasmi visiwani ni Kifiji, Kiingereza na Kihindustani kinachofanana na Kihindi na Kiurdu. Pia kuna lugha nyingine saba za asili (angalia orodha ya lugha za Fiji).

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya Fiji

Fiji ni funguvisiwa iliyoko mbali na visiwa vigine vya Pasifiki. Iko takriban 2.100 km kaskazini kwa Auckland (New Zealand). Visiwa vyake 330 vina eneo la ardhi kavu la 18.270 km².

Fiji ina ukubwa wa kilomita za mraba 194,000, ambapo asilimia kumi tu ya eneo lote hilo ni ardhi, lingine likiwa maji ya bahari ya pasifiki.

Fiji inapatikana katika latitudo 176’ 53” kusini na 178’12” magharibi, lakini pia mstari wa kimataifa wa tarehe unaipa Fiji masaa sawa katika visiwa vyake vyote.

Pia Fiji inajumuisha visiwa vikubwa 322, ambavyo 106 kati ya hivyo vimevamiwa na wakazi ambao si wazaliwa wa eneo hilo, na pia kuna visiwa vingine vidogovidogo zaidi ya mia tano ambavyo pia hujumuishwa katika eneo la Fiji. Lakini kati ya visiwa hivyo ni visiwa viwili ambavyo vimeonekana kuchukua idadi kubwa ya watu ambavyo ni Viti Levu na Vanua levu.ambapo katika visiwa hivi hadi robo tatu ya wakazi wote wa Fiji hupatikana, na ndipo mji mkuun wa Fiji, Suva upo.

Maeneo mengine katika Fiji ni Nandi ambapo kuna uwanja wa ndege wa kimataifa, na Lautoka ambako kuna viwanda na shughuli nyingi za uzalishaji hufanyika hapo. Visiwa hivi vimesheheni milima, kiasi cha kufikia hadi mita 1300 kwa urefu, milima ambayo imetandwa na misitu.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Fiji ilijipatia uhuru wake kutoka katika utawala wa kikoloni wa Uingereza tarehe 10 Oktoba 1970.

Fiji hutawaliwa na Raisi akifutiwa na waziri mkuu, na baada ya hapo hufuatia Mwenyekitit wa Halmashauri ya Machifu.

Wakazi katika visiwa vya Fiji huzungumza lugha za Kiingereza na lugha ya Hindustani, lugha ambayo hufanana na Kihindi na Kiurdu.

Historia ya Fiji, inaonesha kuwa shughuli za ufinyanzi zimekuwepo katika visiwa hivyo kwa muda mrefu, hali inayoashiria kuwepo na ushahidi kuwa Fiji imekuwa ikikaliwa na watu tangu miaka 3500 hadi 1000 kabla ya Kristo.

Japokuwa jamii ya kabila la Lapita ndio wanaoaminika kuwa wa kwanza kuishi katika visiwa vya Fiji, lakini hali hii inatiliwa shaka kutokana na jamii ya kabila la Wamelanesia kuwepo kwa wingi sana katika visiwa hivyo, hali inayoashiria kuwa pengine kabila hilo pia limekuwepo tangu kale,

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa visiwa vya Fiji, wanaaminika kuwa walitokana na Wavivu wa masafa marefu ambao walifika katika visiwa hivyo zaidi ya miaka 3500 iliyopita.

Shughuli za ufinyanzi katika jamii ya watu wa kabila la Lapita zimeonekana kutawala maeneo mengi sana katika visiwa vya Fiji.

Utamaduni katika visiwa vya Fiji umekuwa ukifanana sana na ule wa jamii ya Wamelanesia ambao hupatikana magharibi mwa bahari ya Pasifiki, lakini utamaduni huu umekuwa ukifananishwa sana na ule wa jamii za Samoa na Tonga.

Shughuli za biashara katika mataifa haya matatu yalianza muda mrefu kabla ya kuja kwa watawala wa Ulaya ambao kwa kiasi kikubwa wanaaminika kufika katika visiwa hivyo kwa usafiri wa boti ndogo ndogo maarufu kama kanuu ambazo zinaaminika kuwa zilitengenezwa na wakazi wa visiwa hivyo.

Zana mbalimbali za kufinyangwa zimekuwa zikipatikana katika visiwa vya Samoa na hata katika visiwa vya Marquesas zaidi ya kilometa elfu moja kutoka katika makao makuu ya Fiji.

Fiji inajulikana kama visiwa vya lugha nyingi, kwani lugha tofautitofauti zimekuwa zikipatikana katika visiwa hivyo, hali kadhalika historia ya visiwa hivyo inaonesha kuwepo kwa makabila ambayo yamekuwa yakihamahama kutoka kisiwa kimoja kwenda kingine.

Kwa muda wa karne moja hivi iliyopita, katika visiwa vya Fiji kumekuwa kukiibuka tamaduni tofautitofauti, hali iliyooashiria ubaguzi wa kikabila kuwepo, lakini imekuwa tofauti hii leo, ambapo, wakazi wa Fiji wamekuwa wakiishi kwa amani na wamekuwa wakikielezea kipindi hicho kama kipindi cha “na gauna ni tevoro” yaani "wakati wa shetani".

Mpelelezi wa kutoka Uholanzi aliyejulikana kama Abel Tasman, aliitembelea Fiji katika miaka ya 1643, akiwa anatafuta bara la Afrika kusini lililojulikana kama “the great Southern continent”.

Baada ya uhuru wa Fiji (1970) kutoka kwa Waingereza, yalifuata mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea mwaka 1987, hali iliyosababishwa na wakazi wa Fiji kulaumu serikali yao kutawaliwa na watu wa kabila la Indofijian au Wahindi.

Mwaka 1990, katiba mpya katika utawala wa Fiji iliundwa ambayo ilichukua nafasi ya ile ya awali ambayo ilikuwa ikiegamia upande wa makabila kwa kiasi kikubwa.

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Siasa ya Fiji hufanyika kwa mtindo wa kuchagua wawakilishi bungeni, ambapo waziri mkuu ndiye mkuu wa serikali husika, na rais ndiye mkuu wa visiwa vyote vya Fiji.

Halikadhalika uchaguzi katika Fiji huhusisha vyama vingi ambapo serikali ya Fiji hutawala maamuzi yote ya nchini humo, lakini chini ya demokrasia na utawala wa sheria.

Tangu uhuru katika visiwa vya Fiji kumekuwepo na mapinduzi ya kijeshi mara nne: mara mbili mwaka 1987, mara moja mwaka 2000, na mara moja mwaka 2006, lakini kwa ujumla, jeshi nchini humo limekuwa likishikilia madaraka ya moja kwa moja au kupitia kwa serikali iliyopo madarakani tangu mwaka 1987.

Tarehe 10 Aprili 2009, Rais Iloilo, aliifuta katiba ya nchi hiyo na kufutilia mbali mamlaka ya mahakama akajitangaza kuwa rais wa visiwa hivyo, lakini baadaye alianzisha tena utawala wa kikatiba hali iliyopelekea mwenyewe kutolewa madarakani kwa kubainika alikuwa madarakani kinyume cha katiba.

Tarehe 13 Julai 2009, Fiji ilitolewa katika mkutano wa visiwa vinavopatikana katika bahari ya Pasifiki kutokana na kushindwa kwake kuendesha uchaguzi kwa njia ya kidemokrasia.

Hatimaye tarehe 17 Septemba 2014 uchaguzi huru ulifanyika na kukipa ushindi chama cha FijiFirst (59.2%).

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Idadi kubwa ya wakazi wa Fiji inajumuisha wazaliwa halisi wa Fiji ambapo watu wa kabila la Melanesia huchukua asilimia 54.3 ya wakazi wote wa Fiji, wakati wale wanaojulikana kama Indo-Fijiana huweza kufikia asilimia 38.1, na wengine ni wahamiaji kutoka katika mataifa ya Ulaya waliohamia nchini humo kwa wingi hususani katika karne ya 19.

Lakini kwa ujumla kiasi cha watu wa Kihindi kimekuwa kikipungua siku hadi hadi siku kutokana na wengi kuhama katika visiwa hivyo kwa sababu tofautitofauti, lakini vilevile kumekuwa na kiasi kidogo cha watu kutoka katika visiwa vya Solomoni ambao wengi wao walikuja visiwani hapo kama wafanyakazi.

Imani za dini[hariri | hariri chanzo]

Dini ni moja ya mambo ambayo hutofautisha jamii mbalimbali katika visiwa vya Fiji, hususani baina ya makabila ya Wafiji wenyewe na Wahindi waishio Fiji, ambapo asilimia kubwa ya wenyeji ni Wakristo, wakati watu kutoka India ni Wahindu (70%) na halikadhalika Waislamu (17.9%).

Kwa ujumla dini katika visiwa vya Fiji imetawaliwa na Wakristo ambao ndio wamechukua asilimia kubwa ya idadi ya watu (64,5%), japokuwa Wakristo hawa wanajumuisha madhehebu tofautitofauti kama vile Wamethodisti, Wakatoliki, Wapentekoste, Wasabato na Waanglikana.

Wakazi wa visiwa vya Fiji hujishughulisha na shughuli mbalimbali kama vile uchimbaji wa madini, uvuvi, uvunaji wa mafuta, na biashara.

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Utamaduni katika visiwa hivi hujumuisha tamaduni kutoka makabila tofautitofauti yakiwemo ya Wafiji wenyewe, Wahindi, Wachina na Wazungu ambao kwa ujumla huwa na tamaduni tofatitofauti.

Chakula wanachokula wakazi wa visiwa hivi hujumuisha chakula kitokanacho na mazao ya bahari maarufu kama sea foods, vile vile kuna shughuli tofautitofauti za kitamaduni kama sanaa, uchongaji, muziki na michezo mbalimbali.

Kwa hakika utamaduni wa asili unapewa kipaumbele kama sehemu ya maisha ya kila siku kati wa wakazi wengi, lakini hivi karibuni kumekuwako na mwingiliano wa tamaduni kutoka nchi mbalimbali.

Kwa upande wa sikukuu Fiji husherehekea sikukuu mbalimbali kama vile Mwaka mpya, Maulid, Ijumaa kuu, Pasaka, Siku ya Fiji, Krismasi n.k.

Katika visiwa hivi mchezo mkuu ni Rugby ambapo wachezaji kutoka Fiji wameshiriki mashindano mbalimbali kimataifa.

Kwa ujumla visiwa vya Fiji vimekuwa vivutio kwa watu kutoka maeneo mbalimbali duniani kwenda kwa ajili ya mengi, lakini zaidi mapumziko, hii ni kutokana na hali tulivu iliyopo visiwani hapo, maji maangavu na pia ukarimu wa wakazi wa Fiji.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Serikali
Taarifa za jumla
Safari


Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.