Maelezo ya umma kwenye Facebook ni nini?

Kitu ambacho ni cha umma kinaweza kuonekana kwa mtu yeyote. Hiyo inajumuisha watu ambao si marafiki zako, watu walio nje ya Facebook na watu wanaotumia midia kama vile chapisho, tangazo (mfano: televisheni) na tovuti nyingine kwenye intaneti. Kwa mfano, ukitumia huduma zetu kutoa maoni kwa umma katika muda halisi kwenye kipindi cha televisheni, yanaweza kuonekana kwenye kipindi hicho au kwingineko kwenye Facebook.
je, maelezo yapi huwa kwa umma?
Maelezo unayoshiriki ambapo huwa yapo kwa umma: Baadhi ya maelezo unayotupa unapojaza maelezo ya wasifu wako ni ya umma, kama vile makadirio ya umri, lugha na nchi. Pia tunatumia sehemu ya wasifu wako inayoitwa Wasifu wa Umma, kusaidia kukuunganisha na marafiki na familia. Wasifu wako wa Umma unajumuisha jina, jinsia, jina lako la mtumiaji na Kitambulisho chako cha mtumiaji (nambari ya akaunti), picha kwenye wasifu, picha ya wasifu na picha ya jalada. Pia maelezo haya yapo kwa umma. Baadhi ya njia hii inatusaidia kukuunganisha ni:
  • Jina, picha ya wasifu na picha ya jalada hutusaidia watu kukutambua.
  • Jinsia husaidia watu kukueleza (mfano: "Mwongeze kama rafiki").
  • Kuorodhesha mitandao yako (mfano: shule, eneo-kazi) huwezesha watu wengine kukupata kwa urahisi zaidi.
  • Jina la mtumiaji na Kitambulisho cha mtumiaji (mfano: nambari ya akaunti yako) zipo kwenye URL ya wasifu wako.
  • Safu ya umri husaidia kukupa maudhui yanayofaa kulingana na umri wako.
  • Lugha na nchi husaidia kutoa maudhui na uzoefu unaofaa.
Maelezo unayoshiriki kwa umma: Unapochagua kushiriki kitu kwa Umma (kwa mfano: unapochagua Umma kwenye kiteuzi cha hadhira), inazingatiwa kuwa maelezo ya umma. Ukishiriki kitu na ukose kuona kiteuzi cha hadhira au mpangilio mwingine wa faragha, maelezo hayo pia yapo kwa umma. Jifunze zaidi kuhusu kuhariri ni nani anaweza kuona maelezo msingi kwenye wasifu wako wa Facebook na kutumia kiteuzi cha hadhira kudhibiti unayeshiriki naye unapochapisha kwenye Facebook.
Vitu ambavyo watu wengine wanaweza kushiriki: Watu wengine wanaposhiriki maelezo kukuhusu, hata kama ni kitu ambacho ulishiriki naye lakini hukuweka kwa umma, wanaweza kuchagua kuyaweka kwa umma. Pia, unapotoa maoni kwenye machapisho ya umma ya watu wengine, maoni yako pia yatakuwa kwa umma.
Machapisho kwenye Kurasa za Facebook au vikundi vya umma: Kurasa za Facebook na vikundi vya umma ni nafasi za umma. Mtu yeyote ambaye anaweza kuona Ukurasa au kikundi anaweza kuona chapisho au maoni yako. Kwa jumla, unapochapisha au kutoka maoni kwenye Ukurasa au kikundi cha umma, hadithi inaweza kuchapishwa kwenye Taarifa pamoja na sehemu nyingine kwenye Facebook au nje ya Facebook
Kumbuka kuwa maelezo yaliyo kwa umma yanaweza:
  • Kuhusishwa nawe, hata nje ya Facebook.
  • Kuonekana wakati mtu mwingine anatafuta kwenye Facebook au kwenye injini nyingine ya utafutaji.
  • Kufikiwa kwenye michezo, programu na tovuti zilizojumuishwa na Facebook ambazo wewe na marafiki zako hutumia.
  • Kufikiwa na mtu yeyote anayetumia API zetu, kama vile API ya Grafu.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La