Jina kwenye Facebook

Ili kuhakikisha kwamba watu wanawajua wanaounganishwa nao, tunaomba kila mtu atumie jina wanalotumia katika maisha ya kila leo kwenye Facebook. Huenda tukakuomba uthibitishe kwamba jina lililo kwenye akaunti yako ya Facebook ndilo jina unalofahamika kwalo.
Kuthibitisha jina lako
Ukiona ujumbe wakati unaingia inayokuuliza uthibitishe jina lako, huenda usiwe na uwezo wa kufikia baadhi ya vipengele vya Facebook kwa muda wakati tukishirikiana na wewe kuthibitisha au kuhariri jina lililo kwenye akaunti yako.
Ili kuthibitisha au kuhariri jina lako, ingia kwenye akaunti yako ya Facebook na ufuate maelekezo yaliyo kwenye skrini. Unaweza kuombwa upakie Kitambulisho au kitu kingine kutoka kwenye orodha yetu ya Vitambulisho (m.f: kadi za uwanachama, barua) kinachoonyesha jina unalotumia katika maisha ya kila siku.
Kutumia jina lako kwenye Facebook
Tunaelewa kwamba jina unalotumia kila siku huenda likawa tofauti na jina lako halali. Tunataka utumie jina ambalo wewe hujitambulisha nalo zaidi kwenye wasifu wako wa Facebook.
Kubadilisha jina au kuongeza majina ya ziada
Unaweza pia kubadilisha jina au ukaongeza majina ya ziada (kwa mfano: jina la utani, jina la ukoo la mwanamke aliyeolewa) kwenye wasifu wako. Kumbuka kwamba huwezi kubadilisha jina lako zaidi ya moja ndani ya siku 60.
Kudhibiti faragha yako
Ikiwa una wasiwasi kuhusu kutumia jina lako kwenye Facebook, tuna zana zinazoweza kukusaidia kudhibiti taarifa ambayo watu huona kukuhusu.