Sheria ya Faragha ya Watumiaji ya California itaanza kutumia Januari 1, 2020. Wakazi wa California wanaweza kujifunza zaidi kuhusu haki zao za faragha hapa.

Kampuni ya Facebook sasa ni Meta. Ingawa jina la kampuni yetu linabadilika, tunaendelea kutoa bidhaa zile zile, ikijumuisha programu ya Facebook kutoka Meta. Sera ya Data na Masharti yetu ya Huduma yanaendelea kutumika, na kubadilishwa kwa jina hakuathiri jinsi tunavyotumia au kushiriki data. Jifunze zaidi kuhusu Meta na maono yetu kwa ajili ya metaverse.




Sera ya Data

Sera hii inaelezea maelezo tunayochakata ili kusaidia Facebook, Instagram, Messenger na bidhaa na vipengele vingine vinavyotolewa na Facebook (Bidhaa za Facebook au Bidhaa). Unaweza kupata zana na maelezo ya ziada kwenye Mipangilio ya Facebook na Mipangilio ya Instagram.

Tunakusanya maelezo ya aina gani?

Ili kutoa Bidhaa za Facebook, lazima tuchakate maelezo kukuhusu. Aina za maelezo tunazokusanya zinalingana na jinsi unavyotumia Bidhaa zetu. Unaweza kujifunza jinsi ya kufikia na kufuta maelezo tunayokusanya kwa kutembelea Mipangilio ya Facebook na Mipangilio ya Instagram.
Mambo ambayo wewe na wengine mnayoyafanya na kutoa.
  • Maelezo na maudhui unayotoa. Tunakusanya maudhui, mawasiliano na maelezo mengine unayotoa unapotumia Bidhaa zetu, ikijumuisha unapojisajili kwenye akaunti, kuunda au kushiriki maudhui, na kutuma ujumbe au kuwasiliana na wengine. Hii inaweza kujumuisha maelezo yaliyo kwenye au yanayohusu maudhui unayotoa (kama metadata), kama vile eneo la picha au tarehe ya kuundwa kwa faili. Pia yanaweza kujumuisha unachokiona kupitia vipengele tunavyotoa, kama vile kamera yetu, ndio tuweze kufanya mambo kama kupendekeza barakoa na vichujio unavyoweza kupenda, au kukupatia vidokezo kuhusu jinsi ya kutumia maumbizo ya picha. Mifumo yetu inachakata kiotomatiki maudhui na mawasiliano ambayo wewe pamoja na wengine mnatoa ili kuchanganua muktadha na yaliyomo kwa malengo yaliyofafanuliwa hapa chini. Jifunze zaidi kuhusu unavyodhibiti anayeweza kuona mambo unayoshiriki.
    • Data iliyo na ulinzi maalum: Unaweza kuchagua kutoa maelezo kwenye nyuga zako za wasifu wa Facebook na Matukio ya Maisha kuhusu mitazamo yako ya kidini, mitazamo yako ya kisiasa, "unayempendelea," au afya yako. Maelezo haya pamoja na mengine (kama vile rangi au asili ya kabila, imani za kifalsafa au uwanachama wa muungano wa wafanyakazi) yanaweza kutegemea ulinzi maalum chini ya sheria za nchi yako.
  • Mitandao na miunganisho. Tunakusanya maelezo kuhusu watu, Kurasa, akaunti, alama za reli na vikundi ulivyounganishwa na jinsi ya kuingiliana navyo kwenye Bidhaa zetu, kama vile watu unaowasiliana nao sana au vikundi unavyoshirikiana navyo. Pia tunakusanya maelezo ya mwasiliani iwapo utachagua kuyapakia, kuyalandanisha au kuyaleta kutoka kwenye kifaa (kama vile kitabu cha anwani au kumbukumbu ya simu au historia ya kumbukumbu ya SMS), tunayoyatumia kwa mambo kama kukusaidia pamoja na wengine kutafuta watu ambao mnaweza kuwafahamu na kwa malengo mengine yaliyoorodheshwa hapa chini.
  • Matumizi yako. Tunakusanya maelezo kuhusu jinsi unavyotumia Bidhaa zetu, kama vile aina ya maudhui unayoyatazama au kushiriki; vipengele unavyotumia; hatua unazochukua; watu au akaunti unazoingiliana nazo; na muda; kasi na kipindi cha shughuli zako. Kwa mfano, tunaweka kumbukumbu unapotumia na umetumia mwisho Bidhaa zetu, na machapisho, video na maudhui mengine unayoyatazama kwenye Bidhaa zetu. Pia tunakusanya maelezo kuhusu jinsi unavyotumia vipengele kama kamera yetu.
  • Maelezo kuhusu miamala iliyofanywa kwenye Bidhaa zetu. Iwapo unatumia Bidhaa zetu kwa ununuzi au miamala mingine ya kifedha (kama wakati unanunua kitu kwenye mchezo, au kutoa mchango), tunakusanya maelezo kuhusu ununuzi au muamala. Hii inajumuisha maelezo ya malipo, kama vile nambari yako ya kadi ya mkopo au malipo na maelezo mengine ya kadi; maelezo mengine ya akaunti na uhalalishaji; na maelezo ya bili, usafirishaji na mwasiliani.
  • Mambo ambayo wengine hufanya na maelezo wanayotoa kukuhusu. Pia tunapokea na kuchanganua maudhui, mawasiliano na maelezo ambayo watu wengine hutoa wanapotumia Bidhaa zetu. Hii inajumuisha maelezo kukuhusu, kama vile wakati watu wengine wanashiriki au kutoa maoni kuhusu picha yako, kukutumia ujumbe, au kupakia, kulandanisha au kuleta maelezo yako ya mwasiliani.
Maelezo ya Kifaa
Kama ilivyofafanuliwa hapa chini, tunakusanya maelezo kutoka na kuhusu kompyuta, simu, televisheni zilizounganishwa na vifaa vingine vilivyounganishwa kwenye wavuti unavyotumia ambavyo vinaingiliana na Bidhaa zetu, na tunajumuisha maelezo haya katika vifaa tofauti unavyotumia. Kwa mfano, tunatumia maelezo yaliyokusanywa kuhusu matumizi yako ya Bidhaa zetu kwenye simu yako ya mkononi ili kubinafsisha vyema maudhui (ikiwemo matangazo) au vipengele unavyoona unapotumia Bidhaa zetu kwenye kifaa kingine, kama vile kompyuta ya mkononi au kompyuta kibao, au kupima iwapo ulichukua hatua ya kujibu tangazo tulilokuonyesha kwenye simu yako katika kifaa tofauti.

Maelezo tunayopata kutoka kwenye vifaa hivi yanajumuisha:

  • Sifa za kifaa: maelezo kama vile mfumo wa uendeshaji, matoleo ya maunzi na zanamango, kiwango cha betri, uthabiti wa ishara, nafasi ya hifadhi inayopatikana, aina ya kivinjari, majina na aina za programu na faili, na programu-jalizi.
  • Operesheni za kifaa: maelezo kuhusu operesheni na tabia zinazotekelezwa kwenye kifaa, kama vile iwapo dirisha limewekwa kwenye mandharimbele au mandharinyuma, au mwendo wa kipanya (unaweza kusaidia kutofautisha binadamu na boti).
  • Vitambulisho: vitambulisho vya kipekee, Vitambulisho vya kifaa, na vitambulisho vingine, kama vile michezo, programu au akaunti unazotumia, na Vitambulisho vya Kifaa cha Familia (au vitambulisho vingine vya kipekee kwa Bidhaa za Kampuni ya Facebook zinazohusiana na kifaa au akaunti hiyo).
  • Ishara za kifaa: Ishara za Bluetooth, na maelezo kuhusu maeneo ya karibu ya ufikiaji wa Wi-Fi, violeza, na minara ya seli.
  • Data kutoka kwenye mipangilio ya kifaa: maelezo unayoturuhusu kupokea kupitia mipangilio ya kifaa unachowasha, kama vile ufikiaji katika eneo lako la GPS, kamera au picha.
  • Mitandao na miunganisho: maelezo kama vile jina la opereta wako wa kifaa cha mkononi au ISP, lugha, ukanda wa saa, nambari ya simu ya mkononi, anwani ya IP, kasi ya muunganisho na, katika hali nyingine, maelezo kuhusu vifaa vingine ambavyo viko karibu au kwenye mtandao wako, ili tuweze kufanya mambo kama kukusaidia kutirisha video kutoka kwenye simu yako hadi kwenye televisheni yako.
  • Data ya kidakuzi: data kutoka kwa vidakuzi vilivyohifadhiwa kwenye kifaa chako, ikijumuisha vitambulisho na mipangilio ya kidakuzi. Jifunze zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia vidakuzi kwenye Sera ya Vidakuzi vya Facebook na Sera ya Vidakuzi vya Instagram.
Maelezo kutoka kwa washirika.
Watangazaji, wasanidi programu, na wachapishaji wanaweza kutumia maelezo kupitia Zana za Biashara ya Facebook wanazotumia, ikijumuisha programu-jalizi zetu, (kama vile kitufe cha Kupenda), Kuingia kwa Facebook, APIs na SDK zetu, au pikseli ya Facebook. Washirika hawa wanatoa maelezo kuhusu shughuli zako nje ya Facebook-zikijumuisha maelezo kuhusu kifaa chako, tovuti unazotembelea, ununuzi unaofanya, matangazo unayoyaona, na jinsi unavyotumia huduma zao-iwapo una akaunti ya Facebook au la au umeingia kwenye Facebook. Kwa mfano, msanidi programu wa mchezo anaweza kutumia API yetu kutuambia michezo ipi unacheza, au biashara inaweza kutuambia kuhusu ununuzi uliofanya kwenye duka lake. Pia tunapokea maelezo kuhusu vitendo na ununuzi wako wa nje ya mtando na mtandaoni kutoka kwa watoa huduma wengine wa data walio na haki za kutupatia maelezo yako.

Washirika wanapokea data yako unapotembelea au kutumia huduma zao kupitia wahusika wengine wanaofanya nao kazi. Tunawaruhusu kila washirika hawa kuwa na haki za kisheria za kukusanya, kutumia na kushiriki data yako kabla ya kututolea data yoyote. Jifunze zaidi kuhusu aina za washirika tunaopokea data kutoka kwao.

Ili kujifunza zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia vidakuzi kwa ushirikiano na Zana za Biashara ya Facebook, kaguaSera ya Vidakuzi vya Facebook naSera za Vidakuzi vya Instagram.

Tunatumia vipi maelezo haya?

Tunatumia maelezo tuliyo nayo (kulingana na chaguo unazofanya) kama ilivyofafanuliwa hapo chini na kutoa na kusaidia Bidhaa za Facebook na huduma husiani zilizofafanuliwa kwenye Masharti ya Facebook na Masharti ya Instagram. Hapa pana jinsi ya:
Kutoa, kubinafsisha na kuboresha Bidhaa zetu.
Tunatumia maelezo tuliyo nayo kuwasilisha Bidhaa zetu, pamoja na kubinafsisha vipengele na maudhui (yakijumuisha Taarifa, Mlisho wa Instagram, Instagram Stories na matangazo yako) na kukupa mapendekezo (kama vile vikundi au matukio yanayoweza kukupendeza au mada unazoweza kutaka kufuata) kwenye na nje ya Bidhaa zetu. Ili kuunda Bidhaa zilizobinafsishwa ambazo ni za kipekee na muhimu kwako, tunatumia miunganisho, mapendeleo, mivutio na shughuli zako kulingana na data tunayokusanya na kujifunza kutoka kwako na wengine (ikijumuisha data yoyote iliyo na ulinzi maalum unayochagua kutoa); jinsi unatumia na kuingiliana na Bidhaa zetu; na watu, maeneo, au mambo uliounganishwa nayo na kuvutiwa nayo ndani na nje ya Bidhaa zetu. Jifunze zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia maelezo kukuhusu ili kubinafsisha tajiriba yako ya Facebook na Instagram, ikijumuisha vipengele, maudhui na mapendekezo kwenye Bidhaa za Facebook; pia unaweza kujifunza zaidi kuhusu jinsi unavyochagua matangazo unayoyaona.
  • Maelezo kwenye Bidhaa za Facebook na vifaa: Tunaunganisha maelezo kuhusu shughuli zako kwenye Bidhaa za Facebook na vifaa tofauti ili kutoa tajiriba iliyolengwa na thabiti kwenye Bidhaa zote za Facebook unazotumia, popote unapozitumia. Kwa mfano, tunaweza kupendekeza kuwa ujiunge kwenye kikundi katika Facebook kinachojumuisha watu unaowafuata kwenye Instagram au unaowasiliana nao kwa kutumia Messenger. Pia tunaweza kuboresha zaidi tajiriba yako, kwa mfano, kwa kujaza kiotomatiki maelezo yako ya usajili (kama vile nambari yako ya simu) kutoka kwa Bidhaa moja ya Facebook unapojisajili kwa akaunti kwenye Bidhaa tofauti.
  • Maelezo yanayohusiana na eneo: Tunatumia maelezo yanayohusiana na eneo-kama vile eneo lako la sasa, unakoishi, maeneo unayopenda kuenda, na biashara pamoja na watu walio karibu nawe kutoa, kubinafsisha na kuboresha Bidhaa zetu, pamoja na matangazo, kwa ajili yako na wengine. Maelezo yanayohusiana na eneo yanaweza kuzingatia mambo kama eneo maalum la kifaa (iwapo umeturuhusu kuyakusanya), anwani za IP, na maelezo kutoka kwa matumizi yako na wengine ya Bidhaa za Facebook (kama vile maeneo unayoingia au matukio unayohudhuria).
  • Utafiti na ukuzaji wa bidhaa: Tunatumia maelezo tuliyo nayo kukuza, kujaribu na kuboresha Bidhaa zetu, ikijumuisha kwa kufanya uchunguzi na utafiti, na kujaribu na kutatua bidhaa na vipengele vipya.
  • Matangazo na maudhui mengine yaliyodhaminiwa: Tunatumia maelezo tuliyo nayo kukuhusu-yakijumuisha maelezo kuhusu mapendeleo, hatua na miunganisho yako-kuteua na kubinafsisha matangazo, ofa na maudhui mengine yaliyodhaminiwa tunayokuonyesha. Jifunze zaidi kuhusu jinsi tunavyoteua na kubinafsisha matangazo, na chaguo zako juu ya data tunayotumia kuteua matangazo na maudhui mengine yaliyodhaminiwa kwa ajili yako kwenye Mipangilio ya Facebook na Mipangilio ya Instagram.
Kutoa vipimo, uchanganuzi, na huduma nyingine za biashara.
Tunatumia maelezo tuliyo nayo (pamoja na shughuli yako nje ya Bidhaa zetu, kama vile tovuti unazotembelea na matangazo unayoyaona) ili kuwasaidia watangazaji na washirika wengine kupima mafanikio na usambazaji wa matangazo na huduma zao, na kuelewa aina za watu wanaotumia huduma zao na jinsi ambavyo watu wanaingiliana na tovuti, programu, na huduma zao. Jifunze jinsi ya kushiriki maelezo na washirika hawa.
Kuimarisha usalama, uadilifu na ulinzi.
Tunatumia maelezo tuliyo nayo ili kuthibitisha akaunti na shughuli, kukabiliana na mwenendo hatari, kutambua na kuzuia barua taka na hali nyingine mbaya, kudumisha uadilifu wa Bidhaa zetu, na kuimarisha usalama ndani na nje ya Bidhaa za Facebook. Kwa mfano, tunatumia data tuliyo nayo ili kuchunguza shughuli inayoshukiwa au ukiukaji wa masharti na sera zetu, au ili kutambua wakati mtu anahitaji msaada. Ili kujifunza zaidi, tembelea Kituo cha Usaidizi cha Usalama wa Facebook na Vidokezo vya Usalama wa Instagram.
Wasiliana nawe.
Tunatumia maelezo tuliyo nayo ili kukutumia mawasiliano ya soko, kuwasiliana na wewe kuhusu Bidhaa zetu na kukujulisha kuhusu sera na masharti yetu. Pia tunatumia maelezo yako kukujibu unapowasiliana nasi.
Utafiti na uvumbuzi kwa ubora wa kijamii.
Tunatumia maelezo tuliyo nayo (yakijumuisha kutoka kwa washirika wa utafiti tunaoshirikiana nao) ili kuendesha na kuunga mkonoutafiti na ubunifu kwenye mada za ustawi wa kawaida wa kijamii, uboreshwaji wa teknolojia, mapendeleo ya umma, afya na ustawi. Kwa mfano, tunachanganua maelezo tuliyo nayo kuhusu ruwaza za uhamiaji wakati wa migogoro ili kusaidia juhudi za msaada. Jifunze zaidi kuhusu mipango yetu ya utafiti.

Je, maelezo haya yanashirikiwa vipi?

Maelezo yako yanashirikiwa na wengine kwa njia zifuatazo:

Kushiriki kwenye Bidhaa za Facebook
Watu na akaunti unazosambaza na kuwasiliana nazo.
Unaposhiriki na kuwasiliana kwa kutumia Bidhaa zetu, unachagua hadhira ya kile unachoshiriki. Kwa mfano, unapochapisha kwenye Facebook, unateua hadhira ya chapisho hilo, kama vile kikundi, marafiki zako wote, umma, au orodha ya watu walioteuliwa kukufaa. Vivyo hivyo, unapotumia Messenger au Instagram kuwasiliana na watu au biashara, watu na biashara hizo zinaweza kuona maudhui unayotuma. Mtandao wako pia unaweza kuona hatua ulizochukua kwenye Bidhaa zetu, ikijumuisha ushirikiano na matangazo na maudhui yanayodhaminiwa. Pia tunaruhusu akaunti nyingine kuona waliotazama Facebook zao au Hadithi za Instagram.

Maelezo ya umma yanaweza kutazamwa na kila mtu, ndani na nje ya Bidhaa zetu, pamoja na iwapo hawana akaunti. Hii inajumuisha jina lako la mtumiaji la Instagram; maelezo yoyote unayoshiriki kwa hadhira ya umma; maelezo kwenye wasifu wako wa umma katika Facebook; na maudhui unayoshiriki kwenye Ukurasa wa Facebook, wasifu wa umma kwenye Instagram au jukwaa jingine lolote la umma, kama vile Facebook Marketplace. Wewe, watu wengine wanaotumia Facebook na Instagram, na sisi tunaweza kutoa idhini ya ufikiaji kwa au kutuma maelezo ya umma kwa mtu yeyote ndani na nje ya Bidhaa zetu, ikijumuisha katika Bidhaa za Kampuni nyingine ya Facebook, katika matokeo ya utafutaji, au kupitia zana na API. Maelezo ya umma pia yanaweza kuonekana, kufikiwa, kushirikiwa upya au kupakuliwa kupitia huduma za mhusika mwingine kama vile injini tafuti, API, na midia ya nje ya mtandao kama vile Televisheni, na kwa programu, tovuti na huduma nyingine zinazounganishwa na Bidhaa zetu.

Jifunze zaidi kuhusu maelezo yanayopatikana kwa umma na jinsi ya kudhibiti uonekanaji wako kwenye Facebook naInstagram.
Maudhui ambayo wengine wanayashiriki au kuyashiriki upya kukuhusu
Unafaa kuzingatia unayemchagua kushiriki na yeye, kwa sababu watu wanaoweza kuona shughuli yako kwenye Bidhaa zetu wanaweza kuchagua kuishiriki na wengine ndani na nje ya Bidhaa zetu, ikijumuisha watu na biashara nje ya hadhira uliyoshiriki nayo. Kwa mfano, unaposhiriki chapisho au kutuma ujumbe kwa marafiki au akaunti maalum, wanaweza kupakua, kupiga picha ya skrini, au kushiriki upya maudhui hayo kwa wengine ndani au nje ya Bidhaa zetu, kibinafsi au kwa tajiriba ya ukweli pepe kama vile Nafasi za Facebook. Pia, unapochapisha kwenye chapisho la mtu mwingine au kutoa hisia kwa maudhui yake, maoni au hisia zako zinaonekana kwa kila mtu anayeweza kuona maudhui ya mtu huyo mwingine, na mtu huyo anaweza kubadilisha hadhira baadaye.

Watu pia wanaweza kutumia Bidhaa zetu ili kuunda na kushiriki maudhui kukuhusu kwa hadhira wanayoichagua. Kwa mfano, huenda watu wakashiriki picha yako kwenye Hadithi, kukutaja au kukutambulisha katika eneo kwenye chapisho, au kushiriki maelezo kukuhusu kwenye chapisho au jumbe zao. Iwapo una wasiwasi na kile ambacho wengine wameshiriki kukuhusu kwenye Bidhaa zetu, unaweza kujifunza jinsi ya kuripoti maudhui.
Maelezo kuhusu hali yako ya uamilifu au kuwepo kwako kwenye Bidhaa zetu.
Watu katika mitandao yako wanaweza kuona ishara zinazowaelezea iwapo uko hewani kwenye Bidhaa zetu, ikijumuisha iwapo uko hewani sasa kwenye Instagram, Messenger au Facebook au ulipotumia Bidhaa zetu mwisho.
Programu, tovuti na ujumuishaji kutoka kwa watu wengine kuhusu au kutumia Bidhaa zetu.
Unapochagua kutumia programu, tovuti au huduma nyingine za wahusika wengine ambazo zinatumika, au zimejumuishwa na, Bidhaa zetu, zinaweza kupokea maelezo kuhusu unachochapisha au kushiriki. Kwa mfano, unapocheza mchezo na marafiki wako wa Facebook au kutumia Maoni ya Facebook au kitufe cha Shiriki kwenye tovuti, msanidi wa mchezo au tovuti anaweza kupata maelezo kuhusu shughuli zako katika mchezo au kupokea maoni au kiungo ambacho unashiriki kutoka kwenye tovuti kwenye Facebook. Pia, unapopakua au kutumia huduma hizo za mshirika mwingine, wanaweza kufikia wasifu wako wa umma kwenye Facebook, na maelezo yoyote unayoshiriki nao. Programu na tovuti unazoweza kupokea orodha yako ya marafiki wa Facebook iwapo utachagua kuishiriki nao. Lakini programu na tovuti unayotumia haitaweza kupokea maelezo mengine yoyote kuhusu marafiki zako wa Facebook kutoka kwako, au maelezo kuhusu wafuasi wako wowote wa Instagram (ingawaje marafiki na wafuasi wako wanaweza, bila shaka, kuchagua kushiriki maelezo haya wenyewe). Maelezo yanayokusanywa na huduma hizi za mhusika mwingine zinategemea masharti na sera zao wenyewe, sio hii.

Vifaa na mifumo ya uendeshaji inayotoa matoleo asili ya Facebook na Instagram (km. mahali ambapo hatujaendeleza programu zetu binafsi za mhusika wa kwanza) itafikia maelezo yote unayochagua kushiriki nao, ikijumuisha maelezo ambayo marafiki zako wanashiriki nawe, ili waweze kutoa utendaji wako msingi kwako.

Dokezo: Tupo kwenye mchakato wa kuzuia ufikiaji wa data ya wasanidi programu hata zaidi ili kusaidia kuepusha matumizi mabaya. Kwa mfano, tutaondoa ufikiaji wa wasanidi programu kwenye data yako ya Facebook na Instagram iwapo hujatumia programu yao ndani ya miezi 3, na tunabadilisha Kuingia, ili kwenye toleo linalofuata, tutapunguza data ambayo programu inaweza kuomba bila ukaguzi wa programu ili kujumuisha jina pekee, jina la mtumiaji la Instagram na wasifu, picha ya wasifu na anwani ya barua pepe. Kuomba data nyingine yoyote kutahitaji uidhinishaji wetu.
Mmiliki mpya.
Iwapo umiliki au udhibiti wa sehemu au Bidhaa zote au mali yake itabadilika, huenda tukahamisha maelezo yako kwa mmiliki mpya.

Kushiriki na Washirika wa Wengine
Tunafanya kazi na washirika wengine ambao wanatusaidia na kuboresha Bidhaa zetu au wanaotumia Zana za Biashara ya Facebook ili kukuza biashara zao, ambao huwezesha kuendesha kampuni zetu na kutoa huduma za bila malipo kwa watu kote ulimwenguni. Hatuuzi maelezo yoyote kwa mtu yeyote na kamwe hatutawahi. Pia tunaweka vizuizi vikali kuhusu jinsi washirika wetu wanavyoweza kutumia na kufichua data tunayotoa. Hapa kuna aina za wahusika wengine tunaoshiriki maelezo nao:
Washirika wanaotumia huduma zetu za uchanganuzi.
Tunatoa takwimu zilizojumuishwa na vilivyomo vinavyowasaidia watu pamoja na biashara kuelewa jinsi ambavyo watu wanashirikisha na chapisho zao, uorodheshaji, Kurasa, video na maudhui mengine ndani na nje ya Bidhaa za Facebook. Kwa mfano, wasimamizi wa Ukurasa na wasifu wa biashara ya Instagram wanapokea maelezo kuhusu idadi ya watu au akaunti zilizotazamwa, kutolewa hisia, au kutoa maoni kwenye machapisho yao, vilevile kujumlisha maelezo ya demografia na mengine ambayo huwasaidia kuelewa miingiliano na Ukurasa na akaunti zao.
Watangazaji.
Tunawapatia watangazaji ripoti kuhusu aina za watu wanaoona matangazo yao na jinsi matangazo yao yanavyoendelea, lakini hatushiriki maelezo yanayokutambulisha kibinafsi (maelezo kama vile jina au anwani yako ya barua pepe ambayo kivyake inaweza kutumiwa kuwasiliana na wewe au kukutambulisha) isipokuwa utupatie kibali. Kwa mfano, tunatoa demografia ya kawaida na maelezo yanayopendelewa kwa watangazaji (kwa mfano, kuwa tangazo lilitazamwa na mwanamke kati ya umri wa miaka 25 na 34 anayeishi Madrid na hupenda uhandisi wa programu) ili kuwasaidia kuelewa bora zaidi hadhira yao. Pia tunathibitisha matangazo gani ya Facebook yaliyokufanya ufanye ununuzi au kuchukua hatua na mtangazaji.
Washirika wa kipimo.
Tunashiriki maelezo kukuhusu pamoja na kampuni zinazoyajumlisha ili kutoa uchanganuzi na ripoti za kipimo kwa washirika wetu.
Washirika wanaotoa bidhaa na huduma kwenye Bidhaa zetu.
Unapojisajili ili kupokea maudhui ya malipo, au kununua kitu kutoka kwa muuzaji mwenye Bidhaa zetu, mtengenezaji au muuzaji wa maudhui anaweza kupokea maelezo yako ya umma na maelezo mengine unayoshiriki nao, vilevile maelezo yanayohitajika ili kukamilisha muamala, yakijumuisha maelezo ya usafirishaji na mwasiliani.
Wauzaji na watoa huduma.
Tunatoa maelezo na maudhui kwa wauzaji na watoa huduma wanaosaidia biashara yetu, kama vile kwa kutoa huduma za muundomsingi wa kiufundi, kutathmini jinsi Bidhaa zetu zinatumika, kutoa huduma kwa mteja, kuwezesha malipo au kutekeleza uchunguzi.
Watafiti na wasomi.
Pia tunatoa maelezo na maudhui kwa washirika wa utafiti na wasomi kufanya utafiti unaoimarisha udhamini wa masomo na uvumbuzi ambao unasaidia biashara au lengo letu, na kuboresha ugunduzi na uvumbuzi kuhusu mada za ustawi wa kawaida wa kijamii, maendeleo ya teknolojia, mapendeleo ya umma, afya na ukuaji bora.
Utekelezaji wa sheria au maombi ya kisheria.
Tunashiriki maelezo na watekelezaji wa sheria au katika kujibu maombi ya kisheria katika hali zilizoangaziwa hapa chini.
Jifunze zaidi kuhusu unavyoweza kudhibiti maelezo kukuhusu ambayo wewe au wengine wanashiriki na washirika wengine kwenye Mipangilio ya Facebook na Mipangilio ya Instagram.

Je, Kampuni za Facebook zinafanya kazi vipi pamoja?

Facebook na Instagram zinashiriki muundomsingi, mifumo na teknolojia pamoja na Kampuni nyingine za Facebook (ambazo zinajumuisha WhatsApp na Oculus) ili kutoa tajiriba ya uvumbuzi, muhimu, thabiti na salama katika Bidhaa za Kampuni zote za Facebook unazotumia. Pia tunachakata maelezo kukuhusu katika Kampuni za Facebook kwa malengo haya, kama inavyoruhusiwa na sheria inayotumika na kulingana na masharti na sera zao. Kwa mfano, tunachakata maelezo kutoka kwa WhatsApp kuhusu akaunti zinazotuma barua taka kwa huduma yake ili tuweze kuchukua hatua inayofaa dhidi ya akaunti hizo kwenye Facebook, Instagram au Messenger. Pia tunashughulika ili kuelewa jinsi watu wanatumia na kuingiliana na Bidhaa za Kampuni ya Facebook, kama vile kuelewa idadi ya watumiaji wa kipekee kwenye Bidhaa za Kampuni tofauti za Facebook.

Ninawezaje kudhibiti au kufuta maelezo kunihusu?

Tunakupatia uwezo wa kufikia, kurekebisha, kuweka kituo tarishi na kufuta data yako. Jifunze zaidi katika Mipangilio yako ya Facebook na Mipangilio ya Instagram.

Tunahifadhi data hadi isiwe na umuhimu tena wa kutoa huduma zetu na Bidhaa za Facebook, au hadi akaunti yako ifutwe - litakalotangulia. Huu ni uthibitishaji kesi kwa kesi baada ya nyingine unaotegemea mambo kama asili ya data, kwa nini inakusanywa na kuchakatwa, na mahitaji muhimu ya kisheria au ubakizaji wa operesheni. Kwa mfano, unapotafuta kitu kwenye Facebook, unaweza kufikia na kufuta ulizo hilo kutoka ndani ya historia yako ya utafutaji wakati wowote, lakini kumbukumbu ya utafutaji huo inafutwa baada ya miezi 6. Iwapo utawasilisha nakala ya Kitambulisho chako kilichotolewa na serikali kwa malengo ya uthibitishaji wa akaunti, tunafuta nakala hiyo siku 30 baada ya ukaguzi, isipokuwa vinginevyo kama ilivyofafanuliwa. Tunajifunza zaidi kuhusu ufutaji wa maudhui ulioshiriki na data ya kidakuzi iliyopatikana kupitia programu-jalizi za kijamii.

Wakati unafuta akaunti yako, tunafuta vitu ulivyovichapisha, kama vile picha zako na visasisho vya hali, na hutaweza kujipatia maelezo hayo baadaye. Maelezo ambayo wengine wameshiriki kukuhusu sio sehemu ya akaunti yako na hayatafutwa. Iwapo hutaki kufuta akaunti yako lakini unataka kusitisha kwa muda kutumia Bidhaa, unaweza kulemaza akaunti yako badala yake. Ili kuifuta akaunti yako wakati wowote, tafadhali tembelea Mipangilio ya Facebook na Mipangilio ya Instagram.

Tunaitikia vipi maombi ya kisheria au kuzuia madhara?

Tunayafikia, kuyahifadhi na kuyashiriki maelezo yako na wadhibiti, watekelezaji wa sheria au watu wengine:
  • Katika kujibu ombi la kisheria (kama udhamini wa utafutaji, agizo la mahakama au hati ya kuitwa mahakamani) iwapo tuna imani nzuri ambayo sheria hutuhitaji kufanya hivyo. Huenda hii ikajumuisha kujibu maombi ya kisheria kutoka kwenye mamlaka nje ya Marekani ambako tuna imani nzuri kuwa jibu linahitajika kisheria katika mamlaka hayo, huathiri watumiaji katika mamlaka hayo, na yanaambatana na viwango vinavyotambuliwa kimataifa.
  • Tunapokuwa na imani ya nia nzuri ni muhimu: kutambua, kuzuia na kushughulikia ulaghai, kuidhinisha matumizi ya Bidhaa, ukiukaji wa sera na masharti yetu, au shughuli nyingine hatari au isiyo halali; ili kujilinda (ikijumuisha haki, mali au Bidhaa zetu), wewe au wengine ikijumuisha kama sehemu ya uchunguzi au maulizo ya usimamizi; au kuzuia kifo au madhara ya karibu sana ya mwili. Kwa mfano, iwapo ni muhimu, tunatoa maelezo kwa na kupokea kutoka kwa washirika wengine kuhusu utegemezi wa akaunti yako ili kuzuia ulaghai, matumizi mabaya na shughuli nyingine ya uharibifu ndani na nje ya Bidhaa zetu.
Maelezo tunayopokea kukuhusu, (pamoja na data ya muamala wa kifedha inayohusiana na ununuzi uliofanywa kwa Facebook) yanaweza kufikiwa na kuhifadhiwa kwa muda uliorefushwa wakati ni mada ya ombi la kisheria au jukumu, uchunguzi wa serikali, au uchunguzi unaohusiana na ukiukaji wa masharti na sera unaowezekana, au vinginevyo ili kuzuia uharibifu. Pia tunahifadhi maelezo kutoka kwenye akaunti zilizolemazwa kwa ukiukaji wa masharti kwa angalau mwaka mmoja ili kuzuia marudio ya matumizi mabaya au ukiukaji mwingine wa masharti.

Je, tunaendesha na kuhamisha vipi data kama sehemu ya huduma zetu ulimwenguni?

Tunashiriki maelezo kwa ulimwengu, ndani kwenye Kampuni za Facebook, na nje kwa washirika wetu na wale unaoungana na kushiriki nao ulimwenguni kote kwa uzingatiaji wa sera hii. Maelezo yako yanaweza, kwa mfano, kuhamishwa au kusambazwa kwa, au kuhifadhiwa na kuchakatwa Marekani au nchi nyingine nje ya nchi unayoishi kwa malengo kama ilivyofafanuliwa kwenye sera hii. Uhamishaji huu wa data unahitajika ili kutoa huduma zilizowekwa kwenye Masharti ya Facebook na Masharti ya Instagram na kuendesha na kukutolea Bidhaa zetu ulimwenguni. Tunatumia vifungu wastani vya mkataba, kutegemea maamuzi ya kutosha ya Tume ya Ulaya kuhusu baadhi ya nchi, kama inavyotumika, na kupata ridhaa yako ya uhamishaji wa data hizi nchini Marekani na nchi nyingine.

Tutakuarifu vipi kuhusu mabadiliko ya sera hii?

Tutakufahamisha kabla tufanye mabadiliko kwa sera hii na kukupatia nafasi ya kukagua sera iliyobadilishwa kabla ya uchague kuendelea kutumia Bidhaa zetu.

Ilani ya faragha kwa wakazi wa California

Iwapo wewe ni mkazi wa California, unaweza kujifunza zaidi kuhusu haki zako za faragha ya mtumiaji kwa kukagua Ilani ya Faragha ya California.

Jinsi ya kuwasiliana na Facebook ukiwa na maswali

Unaweza kujifunza zaidi kuhusu jinsi faragha inavyofanya kazi kwenye Facebook na kwenye Instagram. Iwapo una maswali kuhusu sera hii, unaweza kuwasiliana nasi kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Wasiliana Nasi
Unaweza kuwasiliana nasi mtandaoni au kwa barua katika:
Facebook, Inc.
KWA UANGALIFU WA: Shughuli za Faragha
1601 Willow Road
Menlo Park, CA 94025


Tarehe ya Marekebisho ya Mwisho: Januari 11, 2021