Somalia
| |||||
Lugha rasmi | Kisomali | ||||
Mji Mkuu | Mogadishu | ||||
Mji Mkubwa | Mogadishu | ||||
Serikali | Shirikisho la Jamhuri | ||||
Rais | Mohamed Abdullahi Mohamed | ||||
Waziri Mkuu | Mohamed Hussein Roble | ||||
Eneo | km² 637,657 | ||||
Idadi ya wakazi | 11,031,386 (2017) | ||||
Wakazi kwa km² | 17.2 | ||||
Uchumi nominal | Bilioni $7.9 | ||||
Uchumi kwa kipimo cha umma | $716 | ||||
Pesa | Shilingi ya Somalia | ||||
Kaulimbiu | "Soomaaliyeey toosoo"(Wasomali waamke) | ||||
Wimbo wa Taifa | Qolobaa Calankeed (Tuabudu bendera) | ||||
Saa za Eneo | UTC +3 (Wakati wa Afrika Mashariki) | ||||
Mtandao | .so | ||||
Kodi ya Simu | +252 |
Somalia, (kwa Kisomali: Soomaaliya), ambayo inajulikana rasmi kama Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia, ni nchi kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki katika Pembe ya Afrika.
Kijiografia, imezungukwa upande wa kaskazini-mashariki na Ethiopia na Jibuti, na upande wa magharibi ya kati na Kenya; Ghuba ya Aden nayo iko mashariki.
Mji mkuu na mji mkubwa zaidi ni Mogadishu (wakazi 2,120,000).
Jiografia
Historia
Nchi iliunganika mwaka 1960, kutokana na makoloni mawiliː la Waitalia (kusini) na la Waingereza (kaskazini). Baada ya mwaka 1991 nchi ya Somalia ilibaki haina serikali wala umoja wa taifa, iligawiwa na wakereketwa na wanamgambo wa ukoo na eneo, hasa Somaliland, Puntland na Galmudug upande wa kaskazini. Katika miaka 2008-2013 ilihesabika kama nchi filisika. Kwa sasa ni nchi dhaifu lakini inaanza kujengwa upya kama shirikisho.
Watu
Tazama pia: Orodha ya lugha za Somalia
Wakazi asili wa Somalia ni Wasomali (85%) wa makabila yafuatayo:
Wengine (15%) ni:
Kisomali ndiyo lugha ya kawaida ya wakazi wengi na lugha rasmi pamoja na Kiarabu. Kati ya lugha nyingine zinazotumika nchini, mojawapo ni Kiswahili.
Upande wa dini, 99.8% ni Waislamu, hasa Wasuni.
Utawala
Maeneo (umoja: gobolka, wingi: gobollada) ya Somalia, ambayo imegawiwa tena katika wilaya, ni 18:
Mkoa | Eneo (km2) | Wakazi | Makao makuu |
---|---|---|---|
Awdal | 21,374 | 673,263 | Borama |
Woqooyi Galbeed | 28,836 | 1,242,003 | Hargeisa |
Togdheer | 38,663 | 721,363 | Burao |
Sanaag | 53,374 | 544,123 | Erigavo |
Sool | 25,036 | 327,428 | Las Anod |
Bari | 70,088 | 719,512 | Bosaso |
Nugal | 26,180 | 392,697 | Garowe |
Mudug | 72,933 | 717,863 | Galkayo |
Galguduud | 46,126 | 569,434 | Dusmareb |
Hiran | 31,510 | 520,685 | Beledweyne |
Middle Shabelle | 22,663 | 516,036 | Jowhar |
Banaadir | 370 | 1,650,227 | Mogadishu |
Lower Shabelle | 25,285 | 1,202,219 | Barawa |
Bakool | 26,962 | 367,226 | Xuddur |
Bay | 35,156 | 792,182 | Baidoa |
Gedo | 60,389 | 508,405 | Garbahaarreey |
Middle Juba | 9,836 | 362,921 | Bu'aale |
Lower Juba | 42,876 | 489,307 | Kismayo |
Mawasiliano
Mawasiliano ya Jamhuri ya Somalia ilikaribia kuangamia kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini kwa sasa kampuni za binafsi za mawasiliano ya mitambo, zimetwaa karibu miji yote Somalia, na hata kutoa huduma njema kuliko nchi zilizo jirani.
Somalia ni nchi mojawapo Afrika ambayo ina mawasiliano ya bei rahisi zaidi, pengine kwa kuwa Somalia haikuwa na serikali iliyotoza ushuru; (Telecoms thriving in lawless Somalia) Kampuni zinazohudumia watu wa Somalia ni kama:
Tazama pia
- Utamaduni wa Somalia
- Uislamu nchini Somalia
- Waandishi wa Somalia
- Muziki wa Somalia
- Uchumi wa Somalia
- Vita vya Mogadishu
- Mawasiliano nchini Somalia
- Orodha ya kampuni za Somalia
- Jeshi la Somalia
- Usafiri nchini Somalia
- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Marejeo
- Abdullahi, Mohamed Diriye (2001). Culture and Customs of Somalia. Westport, CT: Greenwood Press. ISBN 978-0-313-31333-2.
- Alpers, Edward A. (1976). "Gujarat and the Trade of East Africa, c. 1500–1800". The International Journal of African Historical Studies 9 (1): 22–44.
.
- Gebru Tareke (2009). The Ethiopian Revolution: War in the Horn of Africa. New Haven, CT: Yale University Press. ISBN 978-0-300-14163-4.
- Laitin, David D. (1977). Politics, Language, and Thought: The Somali Experience. Chicago: University Of Chicago Press. ISBN 978-0-226-46791-7.
- Lecarme, Jacqueline; Maury, Carole (1987). "A Software Tool for Research in Linguistics and Lexicography: Application to Somali". Computers and Translation 2 (1): 21–36.
.
- Mauri, Arnaldo, Somalia, in G, Dell'Amore (ed.), "Banking Systems of Africa", Cariplo-Finafrica, Milan, 1971, pp. nbsp;209–217.[1]
- Samatar, Said S. (1982). Oral Poetry and Somali Nationalism. Cambridge: Cambridge University Press. ISBN 978-0-521-10457-9.
- Schraeder, Peter J. (2006). "From Irredentism to Secession: The Decline of Pan-Somali Nationalism", In Lowell W. Barrington, ed., After Independence: Making and Protecting the Nation in Postcolonial and Postcommunist States (pp. 107–137). Ann Arbor, MI: University of Michigan Press. ISBN 978-0-472-09898-9.
- Shay, Shaul. Somalia in Transition Since 2006. Piscataway, NJ: Transaction Publishers, 2014.
- Warmington, Eric Herbert (1995). The Commerce Between the Roman Empire and India. South Asia Books. ISBN 8121506700.
- (1989) Escape from Violence: Conflict and the Refugee Crisis in the Developing World. New York: Oxford University Press. ISBN 978-0-195-05592-4.
Viungo vya nje
- Wikimedia Atlas of Somalia
- Federal Government of Somalia
- Somalia entry at The World Factbook
- Somalia katika Open Directory Project
- Somalia profile from the BBC News
- Habari, mitandao inayojadili kuhusu Somalia.
- AllAfrica.com - Somalia Habari
- International Freedom of Expression eXchange: Somalia Archived Machi 14, 2007 at the Wayback Machine.
- Somalia - A Country Study
- Habari za kawaida
- BBC habari barabara - Somalia: Kutoka kwenye mbomoko?
- interneti- CIA World Factbook - Somalia
- Somali Planet Networks Archived Septemba 27, 2007 at the Wayback Machine.
- US State Department - Somalia includes Background Notes, Country Study and major reports
- Better off Stateless: Somalia Before and After Government Collapse
- Watambuzi
- Anarchy and Invention: Vipi Kampuni za Somalia zaweza kufanya biashara bila serikali? Archived Machi 7, 2008 at the Wayback Machine.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Somalia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |